Mukoba wa Kuwekea Karamu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Hesabu 6:22-27 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake; na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.
Sisi sote tunavyo vitu tunavyomiliki visivyo vya kawaida, vitu tunavyothamini sana. Ndiyo maana tunajaribu kuvitunza vizuri.
Zamani, wakati nilikuwa mwanafunzi mdogo nilipewa zawadi siku ya kusherehekea kuzaliwa kwangu, nilipewa mkoba mpya wa kuwekea karamu na penseli wenye rangi ya kahawia – nadhani haukuwa wa thamani kubwa lakini moyo wangu uliufurahia sana wakati nilifungua karatasi iliyokuwa inaufunika. Mkoba wa kuwekea karamu wa kwangu kabisa, mpya unaopendeza. Jamani!
Kulikuwa upande mmoja kadi ndani ya kuandikia jina juu yake. Hadi leo, sijaandika jina langu taratibu-taratibu kama nilivyoandika siku ile kwenye kadi. Kuandika jina langu juu yake ilizidi kuufanya mkoba ule kuwa na thamani kwangu. Sijui kwa nini tukio lile limebaki kichwani mwangu!
Jana tuligundua kwa pamoja kwamba makusudi ya Mungu kwetu ni mazuri mno. Lakini tunataka kuongeza kingine kilicho muhimu. Tusome tena mistari ile na kuongeza mstari wa 27.
Hesabu 6:22-27 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake; na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia.
Je! Ulielewa ule mstari wa mwisho? Mungu aliahidi kuweka jina lake juu yao, na juu yetu pia. Ndiyo maana Wakristo wanaitwa Wakristo – tumewekewa jina la Kristo mwenyewe. Rafiki yangu, hii ndiyo sababu unaonekana kuwa na thamani kubwa machoni pake akiangalia jinsi maisha yako yanavyoendelea. Wakati Mungu ameshaweka jina lake juu yako, lazima akubariki.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.