Mungu Akubebaye
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 46:3,4 Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani; na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Ulimwenguni ambamo kila kitu kinalenga mafanikio, sio rahisi kutokujiona kwamba hufai. Si tunakusudiwa tuwe watu wenye uwezo na wa kujitegema? Tunakusudiwa tufanikishe mambo yetu, si kweli?
Kwangu mimi, kama mtu aliyezoezwa tangu utoto wake kufaulu daima, imeniletea changamoto kweli maishani mwangu. Sasa kadiri mtu anazidi kuwa na msukumo wa kufaulu na kupata mafanikio, ndipo inavyozidi kumwia vigumu wakati anafeli.
Ni kweli, kinadharia tunafahamu. Ni kweli mtu anajifunza masomo muhimu kwa kupitia makosa yake. Ni njia mojawapo ya mtu kukua hadi awe mtu mzima maishani. Safi kabisa! Lakini haimsaidii wakati ameanguka kabisa; wakati inaonekana kwamba watu wengine wanamdharau na kumhukumu.
Rafiki yangu, lazima tufute mawazo hayo ya mafanikio. Kwa sababu wakati mtu amedhamiria kutafuta uso wa Mungu, ukweli ni kwamba haijalishi ni kipi kinachoweza kumtokea, kama imetoka kwa upumbavu wake au kama kiko nje kabisa ya uwezo wake, Mungu atamvusha.
Hayo ndiyo aliyoweza kuwaambia watu wake Israeli waliomkosea mara nyingi, waliompa kisogo na kumwangusha mara kwa mara:
Isaya 46:3,4 Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani; na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Nisikilize: Utaendelea kufanya makosa mara kwa mara.
Nisikilize tena: Mungu atakuvusha na kukufikisha mahali pa salama hadi uzee wako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.