... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Atakuthibitisha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:8 Ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Mungu Atakuthibitisha


Download audio file

Kustahimili ni neno ambalo hatupendi, wewe na mimi, kwa sababu inamaanisha mateso kupitia majaribu na kuyavumilia mpaka mwisho.  Ni nani anapenda hayo?  Sio wewe, wala mimi, si kweli?

Lakini hata hivi, kustahimimli hua kunahitajika mara kwa mara maishani. Kuna wakati inapendeza kama vile mwanariadha anajisikia vizuri baada ya kuvumilia mazoezi mengi yanayochosha lakini hatimaye yakimletea ushindi na kupewa tuzo.

Lakini pia, kuna wakati hatupendezwi na haja ya kustahimili – mfano, kuvumilia ndoa inayosumbua, shida za uchumi, upweke.  Kuna muda tunakatishwa tamaa na kutaka kuacha kupambana, hatu yule mwanariadha anayeweza kukata tamaa katikati ya mazoezi yake.

Kuna mambo mengi duniani ambayo yanaweza kutushawishi na kutuvuta mbali na Yesu – ufisadi, uchoyo, uongo, ugomvi.  Yaani, jaribu la kuingia mmojawapo ya mambo hayo ni kubwa kiasi kwamba kulipinga linamchosha mtu kabisa.  Yaani ni mapambano kweli.  Lakini sasa, naona ni muda mwafaka kusikia habari njema.  Je!  Uko tayari kuisikiliza?

1 Wakorintho 1:8  Ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Si lazima tuendelee peke yetu, wewe na mimi.  Kwanza, hatuwezi kabisa.  Lakini wakati unamkaribia Yesu, Roho yake atakuthibitisha hata mwisho.  Ili usilaumiwe siku ile Bwana Yesu Kristo atakaporudi.

Hakuna sababu kuendelea peke yako!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.