Mungu Atiaye Moyo Wanaosumbuka
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 7:4b-6 ... Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi. Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. Lakini Mungu, mwenye kufariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwa Tito
Neno “dhiki” si neno linalopendeza, hapana. Ni hali ambayo tusingependa kukumbatia. Lakini, kuna kipindi neno lile linafasiri vizuri sana hali ngumu tunayoipitia.
“Dhiki” ni neno ambalo Mtume Paulo alilitumia zaidi ya mara moja katika nyaraka zake. Kama vile wakati alikuwa anawaandikia rafiki zake huko Korintho:
2 Wakorintho 7:4b … Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.
Ni kweli, haieleweki jinsi anavyotumia neno la dhiki akiongea habari ya faraja na furaha, lakini sentensi hii inatudhihirishia mengi kuhusu Mungu yule aliyemwamini Paulo. Isitoshe, aliendelea kueleza hivi …
2 Wakorintho 7:5,6 Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. Lakini Mungu, mwenye kufariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwa Tito.
Ninafurahi sana kupata fursa hii kukwambia leo kwamba hailishi matatizo unayokabiliana nayo, kwa sababu neno hili ni Neno la Mungu halisi. Ni Mungu akiongea nasi kuhusu faraja na furaha ya Roho yake akitutia moyo wakati nje panakuwa na vita, ndani hofu.
Rafiki yangu. Habari hii ni kwa ajili yako. Mungu anataka ujue faraja na furaha yake. Anataka kukutia moyo katikati ya mateso uliyo nayo. Unaweza kumwamini kutimiza yale aliyeahidi. Umtegemee! Umwendee na kumwomba athibitishe ahadi hii maishani mwako.
Mungu ndiye mwenye kufariji wanyonge.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.