Mwachie Mungu Athibitishe Mipango Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 16:3 Mkabidhi BWANA kazi zako, na mawazo yako yatathibitika.
Sisi sote tunavyo mipango, matazamio, ndoto ambavyo tunazua upya kila mwanzo wa mwaka mpya. Yamkini mwaka huu utakuwa tofauti na miaka mingine, vikawezekana; labda Mungu atatuonekania mwaka huu!
Ni kawaida kabisa katika siku za mwanzoni za mwaka mpya kuwa na mtazamo kama huo; kutafakari upya matazamio yetu na mipango yetu. Je! Vitatimia mwaka huu? Nani anajua? Ni kama bahati nasibu.
Halafu, baada ya kuvitafakari mara kadhaa, kumbe! Tunavirudisha ndani ya kabati na kuendelea na maisha yetu ya kawaida na shughuli zinazotubana na mara moja matazamio yetu, ndoto zetu na mipango yetu vinatoweka. Lakini ingekuwaje kama haikukusudiwa kuwa hivyo?
Mithali 16:3 Mkabidhi BWANA kazi zako, na mawazo yako yatathibitika.
Mara nyingi watu wanasoma mstari huu vibaya, au wanaufafanua visivyo. Wanasema, “Mkabidhi Bwana mipango yako au mawazo yako.” Lakini mstari unasema, “Mkabidhi Bwana kazi zako” – yaani matendo yako, shughuli zako na mambo yote yaliyopo katika maisha yako yanayoweza kusababisha usahau ndoto zako, matazamio yako na mipango yako.
Ina maana, umtwike Mungu kazi zako zote zitoke mikononi mwako, ziwekwe mikononi mwake, uzifanye zote kwa ajili yake yeye, ndipo zitathibitika.
Sasa, ni yapi Mungu anayetaka kutwambia katika haya? Ni kwamba, tukiishi maisha yetu kwa kujitoa kwake na kumtumikia kwa moyo wote, mipango yetu, badala ya kutoweka, itathibitishwa. Kwa hiyo, sikiliza tena …
Mkabidhi BWANA kazi zako, na mawazo yako yatathibitika.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.