Mwana wa Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu hatututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Kadiri mtu anazidi kukomaa, ndipo inatakiwa azidi kuwa na busara. Lakini wakati mtu anazidi kutambua madhaifu yake kupitia changamoto za maisha, kuna kitu kingine kinachoweza kujiinua na kusababisha asipate mafao yote yanayotokana na hekima aliyejifunza. Kile kitu kinaitwa kiburi.
Je! Umewahi kujikuta unadharau watu wengine ukishuhudia ujinga wao, na jinsi hawajakomaa? Je! Kwa kweli, wanaweza kupumbazika hivyo? Labda hukumu yako ni sahihi, lakini dharau yako inatokana na jinsi wewe unajiona kuwa bora; inaleta kiburi pia. Halafu daima, kiburi hakipendezi. Daima.
Nimeona jinsi Wakristo baadhi wamefanya hivyo. Wamefikia hatua ya kumjua Mungu, hatimaye wanashangaa na kukwazika jinsi waulimwengu wanavyoenenda, wakati wao wenyewe walitenda hivyo; halafu sasa wanaharibu yote kwa sababu ya dharau na kujisifu
1 Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu hatutambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Mungu anatupenda kipeo … sasa, tukipokea karama yake ya msamaha inayotolewa bure pamoja na uzima wa milele kupitia imani yetu ndani ya Yesu, jamani, hayo yanabadilisha kila kitu. Na kama imeshakutokea utafahamu ninachokisema.
Lakini kwa wale ambao bado hajajidhirisha kwao, kwa wale ambao hawajapokea karama ile ya neema, hawaelewi, tena hawana uwezo wa kuelewa kwa sababu hawajamjua.
Kwa hiyo usiwashangae. Usione kwamba wewe ni bora. Usiwahukumu, bali uwapende.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.