... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mwanafunzi Aliyekusudia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 14:25-27 Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Maneno “usawa” au “ulinganifu” yanatumika visivyo siku hizi.  Wengi wanatazamia ulinganifu katika matokeo lakini tungepaswa kuhakikisha ulinganifu kwa kila mtu kuwa na fursa ya kujaribu kufanya kitu fulani sawasawa na wengine.

Acha nikuelezee,  Unaamini kwamba kijana aliyekulia katika mazingira duni awe na fursa kuingia chuo kikuu sawasawa na kijana mwingine awaye yote?  Natumaini utakubaliana nami kwamba ni sahihi. 

Lakini tuseme kwamba wanafunzi wawili wanaingia chuo cha uganga, au cha sheria au cha uhandisi na haijalishi mazingira waliyotoka, yakiwa mazuri au duni kabisa, mmoja anajitahidi sana katika masomo yake, lakini ule wa pili ni mvivu, anakuwa mtoro mara kwa mara,  Je, walingane kabisa katika matokeo na maksi? 

Kuna mwanafalsafa Mgriki wa zamani aliyeitwa Aristotle aliandika hivi.  Ustadi si bahati nasibu.  Daima ustadi unatokana na kusudio thabiti, jitihada za kweli, na utendaji mwenye busara. 

Ninakubaliana naye, pia maneno yake yananipelekea kuongea habari ya Wakristo, yaani wafuasi au wanafunzi wa Yesu, haijalishi unawaitaje.  Kila mmoja ana kibali cha kumwendea Yesu sawasawa bila ubaguzi.  Yesu alikufa kwa mara moja tu kwa ajili ya wote. Tusikie anavyosema Yesu mwenyewe kuhusu mada hiyo: 

Luka 14:25-27  Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.  Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 

Ni kweli, Yesu alitia chumvi sana katika kuelezea jambo hilo, lakini mtu hawezi kukosa kumwelewa akijenga hoja: Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy