Mwenendo wa Ujinga na Ukatili
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 73:21,22 Moyo wangu ulipoona uchungu, viuno vyangu viliponichoma, nalikuwa kama mjinga, sijui neno; nalikuwa kama myama tu mbele zako.
Je! Umewahi kutoboa pulizo na sindano? Dakika moja ni pulizo nyekundu nzuri inayoelea angani. Ghafla inapasuka kwa kishindo kikubwa! Inabaki kipande kidogo cha plastiki tu kisichoweza kutikiswa na upepo pale chini.
Mimi nadhani kwamba mara nyingi vipindi vyetu vibaya vinazidi kuonekana kuwa vibaya vikifuata vipindi vizuri sana. Ghafla pulilizo ile nzuri nyekundu ya maisha yetu inatobolewa na sindano. Ghafla kunakuwa kishindo kikubwa halafu mabadiliko makubwa. Yote yametokea na pini ndogo sana, yaani kikero kidogo tu.
Kwa hiyo mtu anajikuta chini kwenye sakafu akiishiwa nguvu na kujiuliza mengi. Ni nini ilitokea na kwa nini? Ingekuaje sasa kama isingetokea hivi ? Je! Ni lini uliwahi kuona matazamio yako na ndoto zako kupasuka hivi? Je! Ulijisikiaje wakati ule?
Ukweli ni kwamba kadiri mtu anashikilia hisia zile, ndipo zinazidi kumwathiri.
Zaburi 73:21,22 Moyo wangu ulipoona uchungu, viuno vyangu viliponichoma, nalikuwa kama mjinga, sijui neno; nalikuwa kama myama tu mbele zako.
Mtu akiendelea kugaagaa kwenye masikitiko ya yaliyotokea, jinsi alivyoangushwa vibaya kutokana na kikero kidogo, lazima atakuwa na uchungu moyoni. Na tukisema ukweli, kama mtu akifikia hali kama hiyo, ataanza kutenda vibaya, vibaya sana – kama mjinga, kama myama mkali.
Usiruhusu matukio mabaya yakufanye uwe na uchungu moyoni. Kwa kweli haina faida yo yote!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.