... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nafsi Moja Moja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 1:28 Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Nafsi Moja Moja


Download audio file

Kama wewe ni mtu anayenifuatilia kila siku kwenye kipindi hiki cha Neno Safi na Lenye Afya –  au ikiwa unanifatilia kwa barua pepe au TV au redio au kwenye mitandao – sijui kama umewahi kujiuliza, je!, lengo kuu la kipindi hiki ni lipi?

Mimi kama mhusika anayeandika kipindi hiki na kukirekodi na kukishuti siku 365 kwa mwaka, hilo huwa ni swali ninalojiuliza mara nyingi kwa sababu sitaki kupoteza muda wangu bure wala muda wako.  Ingekuwa hasara kubwa kama jitihada zote za kuandaa na kusambaza ujumbe wa Neno Safi Lenye Afya duniani kote, kama ingekuwa kazi bure. 

Lakini sio kazi bure kwa sababu ya lengo tulilonalo hapa kwenye huduma yetu ya Christianityworks (yaani Ukristo unafanya kazi kweli kweli).  Lengo linalotusukuma kuandaaa na kurekodi na kusambaza ujumbe huu wa Neno Safi Lenye Afya kila siku: 

Wakolosai 1:28  Ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

Nina shauku kuona kwamba wewe – ndiye, wewe wenyewe! – Yesu zaidi na zaidi kwa kuboresha mahusiano uliyo nayo, mahusiano ambayo yangebadilisha maisha yako.  Pia uwaambie wengine habari za Yesu – na kuwasaidia kwamba na wao wafanye kama unavyofanya. 

Kwahiyo, acha nikutie moyo leo, uwe mwanamume yule au mwanamke yule anayeshikilia sana Neno la Mungu.  Uchunguze sana hekima yake na ushauri wake ili wewe na wale wanaokuzunguka wazidi kuonekana mbele za Mungu kuwa watu waliokomaa kiroho ndani ya Kristo. 

Kwasababu … rafiki yangu, hivyo ndio njia pekee tunayoweza kubadilisha ulimwengu huu, kwa kubadilisha nafsi moja moja. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy