Neema ya Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
Mambo mengi maishani yanatakiwa mtu awe na juhudi nyingi kwa sababu ni kazi ngumu. Ndoa zinazopendeza hazitokei hivi hivi tu, bali zinahitaji wanandoa kujitahidi sana. Kulea watoto ni kazi ngumu vile vile, ni kujituma. Kupandishwa cheo kazini pia ni hivyo hivyo. Nadhani unanielewa, si kweli?
Najiuliza unajisikiaje leo kuhusu mambo yote maishani mwako ambayo yanahitaji kazi ngumu sana siku baada ya siku? Kwa kweli inachosha mtu. Isitoshe, kama wewe ni mfuasi wa Yesu, hata yeye aliahidi kwamba kumwishia sio mchezo, itakuwa kazi ngumu.
Jamani! Ni mzigo! Ni jukumu lingine tena, na hilo linatusukuma kuuliza, … Je! Ninatembeaje na Yesu? Je! Ninatimiza matazamio yake kwa ajili yangu? Itakuaje mwishoni kama sitafai?
Mungu anafahamu kwamba una mambo mengi. Anaelewa unavyosongwa. Lakini swali lile la mwisho ambalo linasumbua watu wengi – Je! Ninafaa au la? – tayari limeondolewa kwako. Mungu mwenyewe ameshachukua mzigo huo, mzigo wenye matokeo yanayoendelea milele, akautoa begani mwako na kuuweka mabegani pa mwingine.
2 Wakorintho 5:21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
Au kama vile A.W. Tozer aliyeeleza, “Dhambi yo yote ile aliyekuwa naye Yesu ilitoka kwetu. Haki yo yote ile tunayoweza kuwa nayo sisi ni ya kwake.”
Wewe na mimi, kwa jinsi tulivyo sisi, kamwe tusingestahili. Lakini wakati tunamwamini Yesu … tayari tumeshastahilishwa. Hii ndiyo neema.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.