Ni Kipi Kitakachopindua Maisha Yako?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 4:12,13,17 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kaperenaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali ... Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Ulimwenguni na hata kwa watu wa Mungu, kuna ujinga mkubwa kumhusu Yesu kwa kile Biblia inachokisema kuwa yeye ni nani, alifundisha nini, na alifanya nini.
Kama hutaki kusumbuliwa ili uendelee na maisha yako ya starehe bila kuwa na changamoto wala madai ni bora uendelee kuishi kwenye ujinga wa kutofahamu asili Yesu. Sitanii. Maisha ya starehe yanaendana na kubuni fikra zako kumhusu Yesu.
Niamini kabisa, nikisema kwamba siku moja mambo yatakuharibikia. Itafika mahala uovu wa ulimwengu huu au dhambi zako zenyewe au vyote viwili vitaungana pamoja na kupindua vibaya maisha yako.
Mathayo 4:12,13,17 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kaperenaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali … Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Bila shaka, swala zima la “toba”, yaani kuachana na mambo unayoyajua kuwa ni mabaya, kuacha sehemu yako ya anasa na starehe wakati mambo yanaenda kombo… yote yatasababisha maisha yako yapinduliwe. Maisha hayawezi tena kuendelea kama ulivyopanga.
Bora kumwachia Yesu arekebisha dira yako ili uelekezwe vizuri kuliko kuacha uovu wako ukuangamize.
Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.