... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kurejeshwa Katika Njia Iliyo Sahihi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Petro 3:8,9 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Listen to the radio broadcast of

Kurejeshwa Katika Njia Iliyo Sahihi


Download audio file

Sasa, ni wakati gani Mungu atakuchoka?  Ni lini atakwambia, “Yatosha! Sitashughulika tena na wewe!?”  Ni wazo linalotisha ambalo nadhani limewahi kupitia kichwani mwako, tena si mara moja.

Ukweli ni kwamba wewe na mimi tuna mwelekeo wa kutaka kumpenda, kumheshimu na kumtii Mungu kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine bado tuna muelekeo wa kuanguka tena kwenye dhambi ile ile ya zamani.  Kama vile Mtume Paulo, tunataka kutenda mema lakini tunashindwa kuyatimiza.

Kadiri hali hiyo inavyoendelea, ndivyo tunavyozidi kutilia mashaka huruma za Mungu na neema yake pia.  Bila shaka, itafika mahala, uvumulivu wa Mungu utaisha.  Labda umeshakatika.

2 Petro 3:8,9  Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.  Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Kwa mtazamo wa milele wa Mungu hakuna utofauti kati ya siku moja na miaka elfu moja.  Kwa hiyo, sasa tunaweza kuelewa vizuri zaidi habari ya uvumilivu wake.  Labda, yawezekana Kristo hajarudi, hajakuita, labda ndio maana bado anakuvumilia, hataki uangamie.

Kamwe usitilie mashaka huruma za Mungu wala neema yake kwako na uvumilivu wake.  Ukianguka, mrudie … mara moja.  Kwasababu ukiishi maisha yako kwa kujua vizuri kwamba bado huruma zile na neema ile, na uvumilivu ule vinaendela kuwepo kwa ajili yako, basi utaelekezwa pole pole ufikilie toba. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.