Ni Yupi Mungu Atakaye mwimarisha?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Mambo ya Nyakati 16:9 Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Kuna tabia moja anayo Mungu ambayo ninaipenda sana, ni nia yake ya kutusaidia na kutupa nguvu wakati sisi tumeishiwa nguvu, kutuvusha mazingira magumu ambayo yangetushinda. Ninapenda tabia yake hiyo.
Isitoshe kuna habari njema nyingine. Mungu mwenyewe anatanguliza msaada wake hata kabla hatujamuomba, ili atupe nguvu, atushindishe katikati ya mazingira yetu.
Ebu fikiria kidogo. Wakati unampenda mtu, wakati unavutwa na masimulizi yake, si unamsogelea na kuinama kwa kumwelekea ili umsikilize vizuri? Wakati hupendezwi na mwingine, unaegamia nyuma kwenye kiti chako, si ndio?
Unajua, Mungu wetu ni Mungu anayeegamia kwa kutuelekea. Yeye ndiye atafutaye wanaohitaji kusaidika. Lakini ukweli ni kwamba kuna kanuni anazofuata ili achague ni nani asaidike. Sikiliza:
2 Mambo ya Nyakati 16:9 Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Acha nieleze kidogo. Huyu Asa alikuwa Mfalme wa Yuda halafu badala ya kumtegemea Bwana wakati alienda vitani, aliomba msaada wa Mfalme wa Shamu; ina maana, hakuwa mwaminifu kwa Mungu.
Sikiliza, Mungu si kwamba anatafuta mtawala, au mwanateolojia mwenye hekima, au mchezaji maarufu au Mkristo bora, hapana. Bali anaridhika kwa kutafuta mtu wa kawaida, watu ambao hawajulikani, watu kama wewe na mimi ambao mioyo yetu imekamilika kwa kumwelekea. Anawatafuta hawa hawa … ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao.
Sasa, kumbuka hayo wakati utajikuta katika hali mbaya. Uwe mwaminifu kwa Mungu na atakuimarisha.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.