Ninachokitaka ni Kimoja tu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:8-10 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake.
Sasa, ninataka kujua ni mambo gani muhimu kwako? Yaani ni kitu gani unakipa kipaumbele kwenye maisha yako ya kila siku!?.
Si swali rahisi kujibu kwasababu, kama Mkristo jibu lako lingekuwa hili … kitu muhimu zaidi ni mahusiano yangu na Yesu. Lakini mara nyingi mambo mengine kama vile kiburi, kutamani kusifiwa na watu wengine, vitu ambavyo tunataka kununua au yale ambayo tunataka tuyafanya, mara nyingi yanajitanguliza mioyoni mwetu kuliko kile kitu kimoja tungechokipa kipaumbele. Tumsikilize Mtume Paulo akifafanua mada hiyo:
Wafilipi 3:8-10 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake.
Yale mengine yote ni takataka ukiyalinganisha na Kristo (katika lugha ya asili imetumia neno “mavi”). Yaani, Paulo alikutana na Kristo, mambo yote yalibadilika kwake.
Ninachotaka sasa ni Kristo … nimjue yeye na uwezo uliomfufua kutoka mautini … niweze kushiriki mateso yake … nifanane naye.
Rafiki yangu, muda umewadia wakukata shauri kabisa kuhusu kile kitu kimoja unachokitaka kweli kweli kwenye maisha haya.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.