Ninatamani…
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 112:5-7 Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya; moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
Je!, Ni lini ulipata jaribu la kutumia udanganyifu? Kwa upande mmoja, ulitambua jinsi ungetenda yaliyo haki. Lakini kwa upande mwingine, kwa kutumia werevu fulani, kwa “kukata kona” au kubana kitu hapa au paleili ujinufaishe.
Jaribu hilo la kulaghai kidogo, kutumia uongo mdogo ili upate unachokitaka, huwa linatokea mara nyingi kuliko tunavyofikiri.
Bila hata kutafakari sana, ungeweza kuona nafasi nyingi tu za kujinufaisha kwa kukandamiza mizani kwa kidole chako.
Kwanini sisi binadamu tunajaribiwa hivyo? Ni kwa sababu tunatamani kupata vitu. Tunatamani mali. Tunataka matokeo tunayoyapenda sisi! Laiti ningepata … Laiti ningeweza … Laiti … Kwahiyo, taratibu taratibu, kwa kutumia uongo, tunajaribu kuelekeza mambo huko tunakotamani.
Zaburi 112:5-7 Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele. Hataogopa habari mbaya; moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
Wakati ule tunapojaribiwa kwa siri, inatakiwa tuwe na ujasiri wa kutenda yaliyo ya haki. Lakini Mungu yupo sirini. Anajua tunapokuwa na msimamo mzuri. Anajua pale tunaposhindwa na majaribu. Halafu kuna matokeo, mema au mabaya yanayotokana na maamuzi yetu.
Kwahiyo … matamanio yako yasipate nafasi kubwa kwenye mahitaji yako, bali uwe na msimamo thabiti wa kutenda yaliyo ya haki.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.