... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ondoa Vya Kale, Ingiza Vipya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 3:11,12 Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu. Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi.

Listen to the radio broadcast of

Ondoa Vya Kale, Ingiza Vipya


Download audio file

Nadhani sote tungekubaliana kwamba kwa ujumla sheria na amri ni nzuri.  Si zote lakini karibia zote.  Lakini amri fulani kwenye kitabu ya sheria ina maana gani kama haiwezi kutekelezwa?

Bila shaka umeshasikia amri fulani kupitishwa lakini ukajiuliza, Je!  Watawezaje kushurutisha amri hiyo itekelezwe?  Kwa kweli kuna mambo mengine ni vigumu kufuatilia, kwa hiyo yanaachwa hivyo hivyo au hatimaye kufutwa kisheria.

Agano la Kale ndani ya Biblia ina sehemu kubwa mbili.  Kwanza kuna sheria ya Mungu, yaani Torati, vitabu vitano vya kwanza – Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu.  Sehemu ya pili ni historia ya jinsi Israeli walivyoshindwa kutekeleza sheria na kuitii.

Kwa hiyo, ilibidi Mungu hatimaye abatilishe mapatano hayo, agano lile na kulibadilisha na jambo lililo bora kabisa.

2 Wakorintho 3:11,12  Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.  Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi.

Mungu alibadilisha utawala wa sheria kwa kuweka kanuni ya neema.  Aliondoa la kale, akaweka jipya.  Alibadilisha masharti ya amri akaweka msamaha kwa kumtuma Yesu kufa kwa ajili yako na kwa ajili yangu. 

Utukufu huo utaendelea milele na milele, ndiyo maana kupitia Roho wake, Mungu anakujaza tumaini leo hii, hapo ulipo, katika maisha haya, tumaini ambalo kamwe haliwezi kukuangusha.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy