Onyo Kali
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Nikwambie kinachonitisha: ni watu wanaojifariji wakijiona kuwa wema tu, wanaoishi kufuatana na “kanuni za kikristo” kwamba watakuwa salama Siku Za Hukumu. Mtazamo kama huo unanifadhaisha kweli!
Kwa nini nina mashaka? Ni kwa sababu imeandikwa hivi:
Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Hicho ndicho kiini cha ujumbe wa Injili. Ni kiini cha Ukristo kwa ujumla. Kwamba mtu hawezi kuokolewa na hukumu na ghadhabu itakayokuja kwa kuishi maisha ya maadili, hapana. Kwamba mtu hatapata kibali cha kwenda mbinguni na kuepuka mateso ya Jehanamu kwa kufuata kanuni za kikristo.
Bali unaweza kuokoka kwa kuweka imani yako ndani ya Yesu tu, yeye aliyekufa pale msalabani ili alipe gharama ya dhambi zako halafu akafufuka tena ili akupe maisha mapya ukiwa na ushirikiano na Mungu ambao utaendelea kukua na kuwa bora zaidi na zaidi katika uzima huu na kuingia uzima utakaokuja.
Watu wengi zaidi wanasimama njia panda kwa swala la kumwamini Yesu. Na hii inanipa hofu kweli kweli. Kama vile mwimbaji maarufu wa Marekani aitwaye Johnny Cash alivyosema, “Nimegundua kwamba hakuna kukaa chonjo kwa swala la mbingu na jehanamu.”
Rafiki yangu, leo ninakupa onyo kali. Maisha yako, na mahali utakapoishi milele yote yako mashakani. Wema na “kanuni za kikristo” haviwezi, nisikilize vizuri, haviwezi – kutosha Siku ya Hukumu. Ni imani ya kweli ndani ya Yesu tu, na kazi aliyokufanyia, imani inayodhihirika kuwa ya kweli ki-utendaj; ukimwishia Kristo, ndio iwezayo kukuokoa. Usikae chonjo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.