Paza Sauti Kutoka Kilele cha Mlima
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Nyakati 16:8,9 Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; zitafakarini ajabu zake zote.
Kuna wakati najaribu kufikiria ilivyokuwa kwa watu pale amani ilipopatikana baada ya Vita ya Kwanza na Vita ya Pili ya dunia. Yaani nafikiri iliwawia vigumu kukubali kwamba kweli amani imerudi. Ni nani hajaona picha za sherehe zilizofanyika baada ya amani kupatikana.
Wazazi wangu waliishi Ulaya wakati wa Vita ya Pili ya dunia. Baba yangu alifanya vita akiwa ndani ya jeshi la Wajerumani lililokabiliana na jeshi la Urusi. Alikuwa kwenye mapambano makubwa ya mji wa Stalingrad wakati anakamatwa na kufungwa katika kambi ya waliotekwa na Waingereza. Hata kama hakupenda kusimulia habari hizo, mimi najua kwamba wakati amani inatangazwa na hatimaye akaachwa huru alijawa na furaha isiyotamkwa.
Inaeleweka vizuri kwa mtu kutkutangaza habari za vitisho vya vita, ila haieleweki kwa mtu kunyamanza kimya asitamke habari za amani.
Sasa, kwanini wengi wanaojiita Wakristo wanaona aibu, huku wakinyamanzia kimya habari njema za Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zetu ile tupate neema na karama ya uzima wa milele? Je! Mtu angewezaje kutokuwaambia watu wengine habari hizo? mmh!
1 Nyakati 16:8,9 Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; zitafakarini ajabu zake zote.
Kwanini watu wa Mungu hawapigi kelele wakipaza sauti juu ya vilele vya milima? Kwanini sisi hatumshukuru na kumwinua kwa mioyo yetu yote kwa sababu ya ajabu zote alizotutendea? Ni nini kilichotufanya tuzizoee tu kana kwamba ni kawaida habari hizi ambazo ni bora mno kuliko kusitishwa kwa vita ya dunia?
Enyi wanadamu wenzangu! Amani tayari imeshatangazwa. Pelekeni habari hizo njema kote duniani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.