Rehema na Kuchukuliana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sabau ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Kwa miaka mingi sasa, utaifa – ambao ni kama ukabila tu – umesababisha matatizo na maumivu mengi, vita na vifo vingi kuliko tuwezavyo kufikiri. Ni Kwanini?
Leo ni siku ya kuadhimisha sikukuu ya nchi mbili zinazotofautiana sana: India wakisherehekea Siku ya Jamhuri, siku waliyopata uhuru kama nchi ya kidemokrasia wakivunja minyororo ya utawala wa ukoloni wa mwingereza. Australia nao tunasherehekea mwanzo wa taifa letu lilipoanza upya, tukikumbuka wakati Wazungu Waingereza walowezi waliposhuka meli kwenye Ghuba Ndogo ya Sydney.
Sherehe mbili tofauti kabisa na kwetu Australia imeleta mgogoro, wengine wakiomba kwamba siku hii inayoitwa Siku ya Australia, ifutwe kwa sababu ya wale walowezi wa kizungu, jinsi walivyowatendea jeuri wenyeji waliotangulia kukaa pale tokea zamani.
Sasa mtu ayafanyaje madai hayo, jamani? Tena si mgogoro uliopo Australia tu, ni tatizo limetokea duniani kote kwa njia mbalimbali. Kwahiyo, swali bado liko pale pale … tatizo hilo litatatuliwaje? Kwasababu mtu akichunguza vizuri, ataelewa msimamo na mtazamo wa kila pande.
Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sabau ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Huruma, unyenyekevu, rehema, uelewano, na msamaha. Pale utambulisho wa watu, iwe wa utaifa au wa ukabila, basi mstari huo ndio jibu la Mungu. Ndivyo tumevyoagizwa tutende kwenye majira haya ya siasa ya utambulisho ambayo yameibuka siku hizi.
Huruma, unyenyekevu, rehema, uelewano na msamaha.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.