... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Roho Mtakatifu Anaondoka na Kutoka Ndani ya Jengo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 3:6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha

Listen to the radio broadcast of

Roho Mtakatifu Anaondoka na Kutoka Ndani ya Jengo


Download audio file

Swali:  Kuna utofauti gani kati ya kufuata amri na kanuni na kumfuata Yesu?  Ni kama hatuwezi kutii amri barabarani, lakini kumfuata Yesu kumbe kunabadilisha mambo yote.  Hii inawezekanaje?

Kupitia historia ya binadamu, watu wamejaribu kushinda uovu – uovu unaotendeka na watu wengine pamoja na uovu unaoibuka kutoka ndani ya mioyo yetu sisi wenyewe.

Kupitia historia, kwa ujumla, watu wamefeli katika jitihadi hizo.  Sisi binadamu tumejaribu mbinu mbali.  Aina mbali mbali za serikali kuanzia udikteta hadi demokrasia, aina mbali mbali ya uchumi kuanzia ukoministi hadi kapitolisma; hata kutumia dini mbali mbali ikiwemo Ukristo.  Lakini hakuna kilichoweza kudhibiti uovu.  Na kuna sababu havikuweza kufaulu.  Ni kwa sababu havikukusudiwa kufanya hivyo!

2 Wakorintho 3:6  Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

Ina maana, amri haziwezi kushinda uovu.  Amri zinaleta kushindwa na hatimaye kifo.  Lakini Roho – Mungu Roho Mtakatifu – yeye anahuisha.  Ndiyo maana dini iliyochina yenye sheria haijaweza kuleta uhuru na uzima, pia haitaweza kamwe!

Kama vile mwimbaji maarufu, Bono wa bendi ya U2 alivyosema, dini ndiyo inayobaki wakati Roho Mtakatifu ameondoka na kutoka ndani ya jengo.

Uwezo uliomo katika yale Mungu aliyotenda wakati alimtuma Yesu kufa kulipa deni la dhambi zetu na kufufuka ili atupe maisha mapya pamoja na Roho Mtakatifu akituhuisha kwa kupulizia uhai wake ndani yetu kwa njia isiyowezekana kwa kufuata kanuni tu.

Kwa maana andiko (sheria) huua, bali roho huhuisha.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy