... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Sehemu Inayotisha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 23:4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Listen to the radio broadcast of

Sehemu Inayotisha


Download audio file

Je!  Wakati vitisho vinakujia, unafanyaje?  Kwa upande mmoja, silika yako ya kukimbilia mahali pa salama lina nguvu kweli.  Lakini kwa upande mwingine, moyoni kabisa, unafahamu kwamba lazima ukabiliane navyo.

Mhusika ninayempenda zaidi kwenye katuni, aitwaye Charlie Brown, aliwahi kutamka hivi, “Hakuna tatizo hata kama lina ukubwa gani ambalo huwezi kulikimbia.”  Hii ni kweli kabisa!  Lakini, je!  Kukimbia matatizo kila wakati, ni busara kweli?

Hapana.  Kuna wakati lazima mtu akabiliane moja kwa moja na mzizi wa tatizo lenyewewe, na akifanya hivyo, mara nyingi itambidi apite mahali pabaya sana ambapo kwa kawaida, asingependelea kupapita.

Zaburi 23:4  Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Penda, usipende, kuna wakati utajikuta unapita kati ya bonde la uvuli wa mauti.  Lakini kuna habari njema.  Mungu yu pamoja nawe mahali pale pabaya, isitoshe, ndipo anakukaribia zaidi.

huna sababu ya kuogopa mabaya.  Hapo hapo ndipo upendo wa Mungu utakuonekania kwa nguvu

Kuna mtu aliwahi kusema hivi, Mtu akielekea pale panapotokea vitisho, wakati anathubutu kutenda kitu kinachomhofisha, hatimaye mtu yule atakuwa anaishia maisha ya hali ya juu ambayo wengine hawafikii.  Ni kweli kabisa.

Lakini hata ikitokeaje ….  hakika wema na fadhili zitakufuata siku zote za maisha yako; na wewe utakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo