... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Sehemu Yako ya Usalama

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 62:7,8 Kwa Mungu wokovu wangu, na utukufu wangu; mwamba na nguvu zangu, na kimbilio langu ni kwa Mungu. Enyi watu, mtumainini siku zote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.

Listen to the radio broadcast of

Sehemu Yako ya Usalama


Download audio file

Jana tuliongea kuhusu mateso – fursa ya kuteswa kwa ajili ya Kristo ili baraka zake zifurike kupitia sisi na kwenda kwa watu wengine, hiyo ni fursa kusema ukweli,  Lakini hata tukijua hilo, bado mateso yanaumiza sana.

Kinachohitajika wakati wa mateso ni kukumbuka ukweli na kuwa na mlango wa kutokea.  Kwasababu, mtu anapoteswa imani yake huwa inalegea kabisa.  Mtu anaanza kuwa na wasiwasi kiasi cha kumtilia mashaka Mungu.  Kwa hiyo, acha nikwambie ukweli alioutumia Mfalme Daudi, mtu aliyeteswa sana kuliko wewe au mimi.  Pia utaona mlango alioutumia yeye kutokea:

Zaburi 62:7,8  Kwa Mungu wokovu wangu, na utukufu wangu; mwamba na nguvu zangu, na kimbilio langu ni kwa Mungu.  Enyi watu, mtumainini siku zote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. 

Lengo ni kwamba, Mungu anataka upate ushindi na heshima pia.  Kwa Daudi, ilimaanisha kwamba ashinde adui na kutawala juu ya kiti cha enzi ya Israeli.  Kwasisi, yani wewe na mimi, labda inamaanisha tofauti kabisa.  Labda ni kusudi tupate ujasiri ambao hatukuwa nao; labda amani ipitayo fahamu wetu. 

Kwa vyovyote vile, ukweli unaosaidia sana ni kwamba, Mungu ni mwamba wako.  Yeye ni kimbilio lako.  Hatikisiki.  Hawezi kukuangusha.  Basi, hiyo inatosha. 

Sasa mlango wa kutumia ambao unasaidia sana ni kuweka tegemeo lako kwa Mungu.  Najua ni rahisi kusema kuliko kufanya, kwahiyo ufunue moyo wako mbele zake.  Mwambie shida zako zote.  Kwa sababu yeye ndiye kimbilio lako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy