... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuzubaishwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 4:7,8 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

Listen to the radio broadcast of

Kuzubaishwa


Download audio file

Kwenye mfumo wa kisasa tunaoishi siku hizi milango yetu ya kuhisi kwamba tumeshambuliwa na mambo mengi ni vigumu sana kukaziwenye kitu kimoja tu.

Kuna ugonjwa wa upungufu wa umakini  siku hizi, ukiunganika na hali ya kukosa utulivu kupita kiasi.  Kwa kiingereza unaitwa Attention Deficit Hyperactivity Disorder (ADHD kwa ufupi).  Ugonjwa huu unasababisha mtu asiwe makini, asitulie, aropoke tu kwa njia isiyoendana na umri wake.  Ndivyo wanavyosema wataalamu wa afya ya akili. 

Siseme kwamba sisi sote tuna huo ugonjwa wa ADHD, hapana, lakini sijui kama umeshaona namna inavyozidi kuwa vigumu kulenga kitu kimoja bila kuzubaishwa. 

Juzi nilimpeleka mke wangu kwenye mgahawa mzuri kwa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa zinazo karibiana mbele yetu.  Ilikuwa muda mzuri kuwa pamoja.  Lakini karibu yetu alikaa mme na mke – si wazee kama sisi – lakini Yule mwanaume alichukua takribani masaa mawili akichezea simu yake huku mke wake akiwa anatazama dirishani tu. Hapo unafikiri mahusiano yao yakoje!? 

Tena hilo si tukio la kipekee.  Watu wengi wana tabia hiyo.  Muda umewadia wakujikagua: 

1 Petro 4:7,8  Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.  Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 

Muda uliobaki ni mfupi, Mwisho wa mambo yote umekaribia kuliko tunavyofikiri.  Kwa hiyo, jirekebishe. Kaza macho, jali watu wengine bila kuzubaishwa.  Jaribu kujali zaidi mahusiano yako na watu wa karibu, kuwa mwenye juhudi katika kupendana.

Pia, nilitaka kusahau, weka simu yako kando, jamani! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.