Shangilia Sasa Hivi!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 5:11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumepokea huo upatanisho.
Baada ya siku chache itakuwa Krismasi. Krismasi yangu. Krismasi yako. Bila shaka tutaisherehekea mahali tofauti kwa jinsi tofauti. Lakini lazima tusherehekee.
Kwa hiyo, hili ndilo swali langu leo: Je! Unajisikia kwamba unataka kusherehekea kweli? Au pengine mafadhaiko ya dunia hii yamesababisha upotee furaha na mshangao tukikaribia Krismasi?
Natumaini kwamba unatazamia kushangilia … lakini haijalishi uko wapi, haijalishi unajisikiaje, kwa moyo wangu wote ninaamini kwamba Mungu anataka usherehekee; anataka ugarikishwe na upendo wake usio na mwisho. Kwa sababu kwa kupitia Yesu, wakati tunaweka tegemeo letu kwake …
Warumi 5:11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumepokea huo upatanisho.
Jana, tulichunguza mistari iliyotangulia na tukasimulia habari ya mpango wa Mungu kutupatanisha tuwe rafiki zake kwa kufuta makosa yetu kupitia dhabihu ya Yesu pale msalabani kwa ajili yetu.
Krismasi ni habari ya Mungu kukusogelea. Krismasi ni habari ya Mungu kukuita kuwa rafiki yake licha ya yale yote uliyoyatenda. Shangilia sasa ! jivunie kupendwa namna hii ya ajabu
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.