... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Siku Zilizorefushwa, Miaka Iliyopunguzwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 13:10,11 Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini.

Listen to the radio broadcast of

Siku Zilizorefushwa, Miaka Iliyopunguzwa


Download audio file

Hata kama takwimu ya kupima urefu wa maisha ya binadamu kwa wastani inaongezeka karibia katika kila nchi duniani, mtu hawezi kutegemea wastani iliyoandikwa ili akadirie muda anaoubakiza hapa duniani.

Siku hizi rafiki yangu wa karibu aitwaye Glenn hakujisikia vizuri, akaanza kupumua kwa shida.  Baada ya kumwendea mganga na kupata vipimo kadhaa, walimkimiza hospitalini kwa oparesheni ya dharura ya kuzibua misipi mitatu inayotoa damu kwenye moyo na kupeleka mwilini.  Jamani, Glenn ana umri wa miaka hamsini tu.

Mimi singemtilia shaka kwamba anaweza kuwa na mishipa iliyoziba. Sasa, tunamshukuru Mungu kwamba amepona vizuri lakini habari yake inathibitisha pointi yangu kwa kusema mtu hawezi kutegemea wastani wa takwimu za utafiti. 

Warumi 13:10,11  Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.  Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. 

Rafiki yangu, huwezi kujua umebakiza muda gani wa kuishi hapa duniani.  Amka!  Ni kipindi muhimu sana.  Muda wa kuonyesha upendo ni sasa!  Kwa sababu mwisho wa mambo, inawezekana kuwa karibu sana kuliko tunavyofikiria.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy