Subiri! Kuna Mengine Tena
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ezekieli 11:19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama.
Nikipiga hatua kila wakati ninaingia mwaka mpya … mara nyingi ninajiuliza kilicho mbeleni. Je! Nitakumbana na changamoto gani mwaka huu? Je! Nitaweza kupambana nazo na kufaulu? Sijui wewe, unafikiri nini?
Tunaishi katika ulimwengu unaothamini utendaji bora. Mtu akifaulu ndipo anapata thawabu. Akifeli, hapati cho chote. Ni mfumo unaowekwa mbele yetu tangu utoto wetu na unathibitishwa siku baada ya siku kwa jinsi ulimwengu unaotutendea.
Je! Ni lini uliwahi kutokufikia kiwango kile kilichowekwa na matazamio ya mtu mwingine? Alikuonaje baada ya wewe kufeli? Nafikiri unanielewa.
Sijui ukoje, lakini kwangu mimi, kwa kina zaidi ninataka kuenenda sawa sawa na jinsi inavyoweza kumpendeza Mungu, nikitenda mema si maovu, nikionyesha upendo kwa watu, si kuwatendea visivyo. Hayo ndiyo makusudi ya moyo wangu kwa ajili ya mwaka huu mpya, tena nayakusudia na moyo wangu wote. Wewe vipi?
Ezekieli 11:19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama.
Kutokana na pendo lake kuu, Mungu ndiye anayetubadilishia moyo, yeye ndiye atupaye Roho yake – Roho Mtakatifu – atuwezeshe kuwa wale aliokusudia tuwe wakati alituumba. Hauna haja kujitahidi peke yako, hapana. Msaidizi wako mkubwa ni Mungu mwenyewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.