Swala Lisilotiliwa Maanani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Tito 1:8 Bali (mzee wa kanisa) awe mkaribishaji, mpenda mwema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake.
Kadiri ninavyochunguza maisha ya watu, ndipo ninaguswa sana kuona hali halisi kwamba hakuna asiye na matatizo maishani mwake. Vipi wewe?
Ni kweli, kuna wakati mambo yako shwari. Lakini baada ya muda mfupi tu, panazuka upinzani, mapambano, mgogoro fulani, si kweli?
Kipindi kama hicho, sisi sote tungependa kuwa na mtu kutuunga mkono, sisi sote tungependa kuwa na rafiki wa kuongea naye. Na tukigeuza mtazamo kidogo sisi wenyewe tungeweza kuwa yule anayeunga mkono kuwa rafiki mtu yule mwingine akipata shida.
Je! Lazima nifanye hivyo? Kwa kweli siyo vigumu kama unavyofikiria.
Mtume Paulo alikuwa anamwandikia rafiki yake Tito kuhusu sifa ya kiongozi wa kanisa – halafu katika orodha hiyo kuna jambo fulani ambalo ni rahisi kutokuliona.
Tito 1:8 Bali (mzee wa kanisa) awe mkaribishaji, mpenda mwema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake.
Ni kweli, lazima mzee awe mwenye haki, mwenye hekima, mtu anajitolea, anayempendeza Mungu na mtu ajuaye kuthibiti nafsi yake. Haya yote yanaeleweka vizuri. Lakini sifa inayosahaulika mara nyingi ni ipi? Mzee wa kanisa awe mkaribishaji.
Yaani, ni kuwa mkarimu. Kukaribisha mtu kuchangia kikombe cha chai au kahwa, kutumia chakula kwa pamoja, kuwa na mazung’mzo. Mara nyingi hayo machache yanatosha. Uwe tayari kukaribisha watu nyumbani mwako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.