... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tenda Fadhili, Uwe Mkarimu, Tenda Kwa Haki

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 112:5,6 Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele

Unajua ninavyofikiri?  Ninafikiri kwamba ni rahisi kuufanya Ukristo kuwa swala la kiroho tu.  Kuvutwa na kuimba nyimbo na kusalimiana – Bwana asifiwe ndugu! – hadi tunasahau kwamba upendo pamoja na kuwa nomino ni neno la kitenzi pia.

Katika tamaduni zote neno upendo si kitu tulicho nacho tu au kukikosa, yaani nomino tu, bali ni kitu ambacho kinachotupasa kufanya, yaani kitenzi pia.

Sisi sote tunapenda kupendwa.  Lakini tunaonyesha upendo kiasi gani kwa watu wengine kiutendaji?  Kwa kusaidia mtu, kwa kumwunga mkono … kuonyesha uaminifu na uadilifu kazini.  Ninamfahamu mfanya biashara anayeonekana kuwa mcha Mungu, mtu anayependeza Jumapili, lakini kazini ni bosi anayetawala kwa mabavu, ndiyo maana wafanyakazi wake hua hawakai, daima anahitaji kutafuta wengine.

Zaburi 112:5,6  Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki.  Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele.

Sijui – nadhani inawezekana mtu kulenga mambo ya kiroho tu katika swala la kumwamini Yesu na kusahau mambo ya kawaida na matatizo ya kiutendaji.  Mambo hayo ndiyo watu wengine wanayaangalia.  Ni mambo ambayo yanaweza kuwaonyesha upendo wa Mungu huyu tunayekiri kwamba tunamwamini.  Yakikosekana, basi hawatauona.

Sasa kama unaona, kwamba tumezidi kukazia mada hii wiki hii, basi ujue kwamba nimeifanya kwa makusudi.  Kwa sababu Mungu anaona kwamba utendaji katika upendo ni muhimu sana.

Heri atendaye fadhili na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa haki.    

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy