Tumaini Lako Liwe Ndani ya Bwana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 3:18,19 Ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Rafiki anayekuonekania wakati wa tatizo ni rafiki kweli kweli. Kweli hakuna jambo jema kama kuwa na mtu ambaye unaweza kumtegemea, mtu ambaye anakutetea, mtu anayekupenda na kukujali wakati unapitia kipindi kigumu. Hakuna!
Mimi ninakumbuka wakati nilikuwa ninapitia kipindi kigumu mno karibia miaka thelathini iliyopita – kigumu kiasi nilitamani kujiua tu – Mungu aliniletea watu wema kabisa. Lakini hata wao hawakuweza kufikia kwenye kiini cha moyo wangu na kutoa maumivu yangu. Ni katika mazingira yale mabaya nilikutana na Yesu kwa mara ya kwanza. Yeye ndiye aliyekuwa nuru pekee iliyoangaza bila kukoma katika giza ile nene.
Ebu tuchunguze sehemu ya pili ya dua Paulo aliyo omba kwa ajili ya rafiki zake …
Waefeso 3:18,19 Ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Jamani! Ni dua moja ya hali ya juu kabisa!
Upendo upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Hili ndilo dua ninaloomba kwa ajili yako pia. Kwa sababu ninaweza kukwambia kwamba siku zile zenye giza zinazotujia sisi sote, ufahamu wa ukubwa wa upendo wa Mungu kwako ndani ya Yesu Kristo, ni jambo pekee kabisa liwezalo kukuponya na maumivu yako.
Ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.