... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tuondokane na Upumbavu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Tito 3:3,4 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa.

Listen to the radio broadcast of

Tuondokane na Upumbavu


Download audio file

Hakuna apendaye kuonekana kwamba hana akili, lakini hata hivi, sisi sote tumewahi kupumbazika na kutenda mambo ya ajabu ajabu.  Na kila wakati tunatenda yasiyofaa ni kwa sababu tumetanguliza tamaa zetu kuliko yale tuliyoyatambua kuwa ya haki.  Hii ni njia ya upumbavu iliyozoeleka.

Tunafahamu vema kwamba yatupasa kuwa wafadhili, lakini kuna wakati mtu anachoshwa, anaweza kumfokea mtu mwingine.  Tunajua pia kwamba inatupasa kusamehe, lakini mtu anaweza kuwa na kinyongo moyoni miaka mingi.  Tunapaswa kuwa waadilifu … lakini wakati mwenye duka anadanganyika na kukurudishia chenji iliyozidi, je!  Si rahisi kuiweka mfukoni na kuondoka tu?

Matendo kama hayo ni ya upumbavu, kwa sababu hatimaye wewe na mimi, tutapaswa kutoa mahesabu mbele ya Mungu kwa ajili ya matendo yetu yote.  Ni upumbavu kweli! 

Tito 3:3,4  Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.  Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa. 

Wakati wema wake Mungu na upendo wake kwetu unatufikia, kumbe!  Kunatokea jambo la ajabu lenye nguvu kabisa.  Mistari inayofuata yale tuliyoyasoma inatwambia kwamba Mungu alituokoa kwa huruma zake.  Inaeleza pia jinsi anatuosha na kutufanya wapya akitumwagia Roho wake Mtakatifu kupitia Yesu. 

Sasa kazi hii ya Mungu aokoaye, yenye rehema ni dawa ya kutibu upumbavu unaokuwapo katika asili yetu kama wanadamu.  Acha wema na upendo wa Mungu Mwokozi usababishe uondokane kabisa na upumbavu wote.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy