Tusitumie Vifaa Vibutu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 14:5-7 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
“Kweli” ni dhana inayovutia. Tunaelewa kwamba ni dhana isiyo na upendeleo – yaani jambo fulani ni kweli ama si kweli. Lakini hata hivi inaweza kukwaza mtu hadi asitake kuipokea.
Zamani nilikuwa nimenenepa sana kupita kiasi na nilianza kuugua kisukari. Nilikuwa hatarini kwa kweli. Wakati ule nilianza kujiangalia kwenye kioo sikutaka kujipiga picha.
Ni wazi kwamba kuna utofauti katika ya kujua ukweli na kuukubali; kati ya kuukubali kichwani na kuuruhusu ubadilishe maisha yetu. Huwezi kumpiga mtu kichwani ukitumia kweli halafu utazamie abadilike. Ndiyo maana Mungu aliamua kufanya Kweli … kuwa nafsi, yaani mtu.
Yohana 14:5-7 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
Yesu hakusema, “Njia ni huko, kule …” Bali alisema, “Mimi ndimi njia.” Hakusema, “Hii ndiyo kweli,” akitaja orodha ya masharti na kanuni ambazo zingewachanganya watu waliokuwa wameonewa wakati ule. Alisema, “Mimi ndimi kweli.”
Sasa, ikiwa Mungu ameifanya kweli kuwa swala la mahusiano kati ya watu, yamkini ingekuwa jambo la busara sisi kuitumia hivyo wakati tunajaribu kuwaambia watu ukweli wa Habari Njema ya Yesu.
Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. Yesu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.