... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tusiwatupie Watu Mawe

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 8:7,10,11 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe ... Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usetende dhambi tena.

Listen to the radio broadcast of

Tusiwatupie Watu Mawe


Download audio file

Tukimwona mtu mwingine akitenda mabaya, mara nyingi tunafikiri ni wajibu wetu kumtupia mawe.  Ni huzuni kabisa kwa sababu mwitikio huo unaonekana zaidi kwa Wakristo kuliko watu wa kawaida.  Kwa nini?

Labda ni kwa sababu mtu aliyedhamiria kumfuata Yesu hua ana hisia kali kutenganisha mema na mabaya.  Sasa kadiri hisia hiyo ya kutenganisha mema na mabaya inavyozama ndani yetu, ndipo tunavyoweza kuzidi kuhukumu matendo maovu yanayotendeka na watu wengine.

Zamani, viongozi wa dini walimburuta mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakimleta mbele ya Yesu ili wamjaribu.  Sheria ya Wayahudi ilisema kwamba apigwe mawe mpaka afe.Sheria ya Warumi ilisema kwamba Mkuu wao wa Mkoa peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kupitisha hukumu ya kifo.  Ilikuwa mtego kweli!

Yohana 8:7,10,11  Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe … Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako?  Je!  Hauna aliyekuhukumu kuwa na hatia?  Akamwambia, Hakuna, Bwana.  Yesu akamwmabia, Wala mimi sikuhukumu.  enenda zako; wala usitende dhambi tena.

Ebu fikiria.  Yule mmoja aliyekuwepo pale asiye na dhambi, yule mmoja aliyekuwa na sifa ya kumtupia jiwe, aliamua kuacha!

Kujikumbusha:  Usiwatupie wengine mawe.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy