Tutiane Moyo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waefeso 5:19,20 Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Bila shaka umewahi kukatishwa tamaa halafu anakuja mtu akikwambia neno la kukutia moyo na mara moja unakuta amekuinua na kubadilisha hali yako ya siku ile au hata kubadilisha maisha yako.
Kwa hiyo tujaribu kufikiria kwamba kama leo au kesho, wewe na mimi tungekuwa mtu yule anayemtia moyo mwingine. Kwa sababu kama tunajiita Wakristo, kama tunamwamini Yesu, basi Roho Mtakatifu ana shauku kubwa ya kutujaza tele furaha hata kufurika.
Halafu hayo mafuriko yataweza kuwaletea uzima wengine wengi wanaotuzunguka, wale wanaoumia na kuwa na kiu moyoni. Ni kweli, mara nyingi hatujisikii kama tuna furaha ya kutosha , Lakini sikiliza maneno yafuatayo:
Waefeso 5:19,20 Mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Nyimbo na muziki ni kipawa kizuri sana kitokacho kwa Mungu. Nyimbo za redioni au kwenye mtandao, mtu anaweza kusikiliza tenzi na nyimbo zenye nguvu. Tena Mungu hajali kama hauna sauti nzuri ya uimbaji kama wengine, bado anapenda kusikia unamwimbia sifa zake. Anafurahi sana wakati unatengeneza wimbo moyoni. Anapendezwa sana ukimshukuru kwa kila jambo katika jina la Kristo!
Ukifikia hapo, basi hutaweza kujizuia. Mafuriko ya furaha yatakutoka na kuwatia moyo wahitaji wanaokuzunguka!
Imba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.