Imani Bure
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 15:11-14 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
karne na karne, ufufuko wa Yesu umejadiliwa sana kama ni kweli au si kweli? Hata leo wengi wanalichukulia kama jambo lililobuniwa na watu tu. Wewe unaamini kama mtu anaweza kufufuka kutoka wafu!?
Unajua, kuna watu wengi leo wanajiita Wakristo lakini hawaamini kama Yesu alifufuka kimwili kweli kweli, au wanaona kwamba ni jambo geni kabisa kiasi cha kulipuuza (hawataki hata kulifikiria hata kama hawalikani).
Lakini hali hiyo si mpya, ilianza punde tu Yesu alipofufuka baada ya kutembea hapa duniani na kusulubiwa. Sikiliza Mtume Paulo alivyoandika kuhusu swala hilo:
1 Wakorintho 15:11-14 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.
Anaongea moja kwa moja bila kuficha, Kama Yesu hakufufuliwa kutoka kwa wafu, basi hata wewe na mimi au mwingine yoyote anayemwamini hawezi kupata ahadi yake ya uzima wa milele.
Ufufuko wa Yesu si jambo ambalo mtu anaweza kulipuuza, isipokuwa, akitaka kukosa uzima wa milele.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.