Uhuru wa Kweli
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wakorintho 3:17,18 Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Je! Ungependa kuwekwa huru na mzigo wa dhambi? Nadhani sisi sote tunayo shauku kuwa huru nayo. Sasa habari njema ni kujua kwamba ni kwa sababu iyo hiyo Yesu alikuja hapa duniani. Ili akuweke huru.
Je! Njia iendayo kwenye uhuru inafananaje? Sisemi kinadharia bali kiutendaji. Siulizi habari ya maisha ya watu wengine, bali maishani mwako wewe? Usisite, niambie, inafananaje? Basi, sikiliza sasa mtazamo wake Mungu … kuhusu uhuru wako:
2 Wakorintho 3:17,18 Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Mtu awaye yote aliyemwamini Yesu – mtu anayeishi maisha ya imani, akiamini kwamba Yesu ni yeye yule aliyedai kuwa, alikufa kulipa deni la dhambi zake, kwamba alifufuka tena ili ampe maisha mapya, uzima wa milele – tayari ameshampokea Roho Mtakatifu. Sasa alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
Kwa hiyo, uhuru si kitu ambacho unakitumikia au kukitafuta mwenyewe, bali ni kipawa cha Mungu kupitia uwepo wake ndani yako, kila dakika ya kila siku kwa maisha yako yote.
Haya yote yanatokana na Bwana, aliye Roho. Hii ni habari njema.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.