... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uishie Imani Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 1:5,6 Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.

Listen to the radio broadcast of

Uishie Imani Yako


Download audio file

Acha nikuulize swali ambalo litakusumbua.  Kama wewe ni mtu anayemwamini Yesu, je!  Unawezaje kujua kwamba imani yako ndani yake ni ya kweli?  Kwa sababu kuna siku ambazo imani yako inaonekana kuwa dhaifu, sindiyo?

Angalia, siku kama hizi hua zinatujia sisi sote, ikiwemwo na mimi pia.  Labda utashangaa kusikia mhubiri anakiri hivyo, lakini ndivyo ilivyo.  Lakini kinachonifurahisha katika hali hiyo ni kukumbuka kwamba mambo hayategemei ukubwa wa imani yangu – imani saizi ya mbegu ya haradali ndiyo Yesu anataka aone. 

Lakini baada ya kusema hayo, bado kuna kitu ambacho tunaweza kufanya, wewe na mimi kuondoa kabisa mashaka na kutuongoza kupiga hatua mbeleni katika ushindi na kuingia katika mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yetu.  Tusikilize tena busara ya mzee Mtume Paulo akimwandikia kijana Timotheo: 

2 Timotheo 1:5,6  Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.  Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 

Kwa kifupi, imani pasipo matendo imekufa.  Ndiyo maana Mungu anataka ukumbuke karamu aliyokupa.  Yaani kipawa kile cha kipekee, kipaji ulicho nacho cha kutimiza jambo fulani vizuri kuliko mtu mwingine awaye yote.  Na kwa sababu unazoeza karama ile kwa kuitumia kubariki wengine kwa ajili ya utukufu wake Mungu, kumbe!  Ndipo moto ule mdogo wa imani yako utachochewa kabisa na kuwa mkubwa! 

Usisahau kuchochea na kutumia karama Mungu aliyokupa! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy