... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ujumbe Uliotoka Mwanzo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 3:11-13 Maana, hii ndiyo habari mliyosikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi. Si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

Listen to the radio broadcast of

Ujumbe Uliotoka Mwanzo


Download audio file

Pendo ni neno rahisi.  Halafu ukitafakari habari ya kupendwa – kupendwa na wapendwa wako na kupendwa na Mungu – ni jambo linalopendeza sana kuliko yote.  Kwa nini basi, mara nyingi tunaharibu mambo?

Kinachohuzunisha ni kwamba leo hii, kuna watu wengi duniani ambao hawajisikii kwamba wanapendwa hata kidogo; pengine waliwahi kupendwa lakini sasa wamekataliwa.  Mimi binafsi nilipitia hali hiyo.  Ninaelewa vizuri hali ya upweke na maumivu yale makali.  Sasa kwa mtu awaye wote anajisikia hivi muda huu huu, jua kwamba Mungu anaumia sana kwa ajili yako.

Lakini hatuongee ukosefu wa upendo tu.  Tujue kwamba chuki ni kinyume cha pendo.

1 Yohana 3:11-13  Maana, hii ndiyo habari mliyosikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi.  Si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake.  Naye alimwua kwa sababu gani?  Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

Kinyume cha chuki hii kubwa, kuna yale ambayo mtu aitwaye Augustine aliwahi kusema,  Kwa kuwa pendo linaweza kukua ndani ya mtu, uzuri na wenyewe unaweza kuzidi kuonekana.  Kwa sababu pendo ni uzuri wa nafsi ya mtu.

Rafiki yangu, katikati ya chuki, vikundi, ukosefu wa upendo maishani mwa watu wengi, wewe na mimi tunaweza kuwa watu ambao tunaoupitisha uzuri wa pendo la Mungu.  Kuna wakati itakuwa wewe tu unaoweza kufanya hivi.  Je!  Ni yupi ambae Mungu anakuita leo uweze kumpenda?  Maana, hii ndiyo habari mliyosikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.