... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umsifu kwa Shauku Kubwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 150:1-6 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi; msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.

Listen to the radio broadcast of

Umsifu kwa Shauku Kubwa

Download audio file

Je!  Naweza kukuuliza ni lini uliwahi kumsifu Mungu?  Na wakati ulimsifu, ulifanyaje?  Haya ni maswali mazuri ya kujiuliza siku ya Jumapili wakati Wakristo duniani kote hua wanakusanyika kwenye ibada ya kumwabudu Mungu.

Je!  Ni mara ngapi umekuwa ibadani ukiimba wimbo wa sifa au wa maabudu lakini badala ya mawazo yako kumlenga Mungu, umeyaruhusu kuzurura?  Halafu, familia fulani wakiingia chelewa, na bado maneno ya sifa yakiwa midomoni mwako, uligeuza kichwa na kuwatazama kwa macho yako na kufikiri, Wale njamaa, daima wanachelewa.  Wana matatizo gani?!

Lazima ujiulize, Je!  Kwa kweli ninamsifu Mungu aliyemtuma Mwanae aniokoe?  Tujikague sasa tukisikiliza Zaburi ya mwisho ndani ya Biblia:

Zaburi 150:1-6  Haleluya.  Msifuni Mungu katika patakatifu pake; msifuni katika anga la uweza wake.  Msifuni kwa matendo yake makuu; msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.  Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi; msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana.  Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.  Haleluya.

Nikitafakari zaburi hii, maneno ambayo yananijia kichwani kwa kueleza aina ya sifa mtunga zaburi ana taja hapa, ni maneno kama kufurahia, shangwe na shauku.  Je! Ndivyo unavyomsifu Mungu?  Kwa sababu nadhani hajali sana mlingano wa sauti yako, hapana.  Anachokijali ni yale yaliyomo moyoni mwako.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy