... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Umsifu Yeye Bwana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 86:12,13 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, kwa moyo wangu wote, nitalitukuza jina lako milele. Maana fadhili zako ni nyingi sana; umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

Listen to the radio broadcast of

Umsifu Yeye Bwana


Download audio file

Kwa sehemu kubwa, jinsi mtu anavyopitia maishani – atakayoyapata, atakayoyatoa, atakayafurahia au la … inategemeana na mtazamo unaomtawala yeye.  Nafikiri tungekubaliana kuhusu watu aina tatu – wa kwanza aliye na mtazamo wenye harara, wa pili ni mtu anajiona daima kuwa mwathiriwa, wa tatu mtu mwenye shukrani – kwamba watakuwa wana mitazamo tofauti kabisa kuhusu ulimwengu wetu na matukio yanayowafikia maishani.

Angalia, hisia zetu hua zinapanda na kushuka.  Kuna wakati tunakatishwa tamaa, kuna wakati tunachangamka.  Hii ni kawaida tena si vibaya.  Lakini swali nyeti ni hili: Je!  Mtazamo unaokutawala maishani ni upi?

Je!  Daima unajifanya kuwa mwathiriwa?  Je!  Mtazamo huo umekusaidiaje?  Nikikuuliza bila kukwepa, je!  Wewe una kiburi  Je!  Unalazimisha wengine?  Je!  Uhusiano wako na watu wengine ukoje?  Je!  Daima uko mwenye harara, usiweze kuridhika hata ukiambiwa nini au utendeweje?  Je!  Mtazamo wako unakuletea furaha kweli?  Nafikiri umenipata.

Kwa hiyo, acha nikuulize leo, Je!  Mtazamo unaokutawala moyoni kuhusu maisha yako, mazingira yako, familia yako, kazi yako ni upi? Sasa wakati unatafakari maswali yangu, acha maneno mazuri yafuatayo yajae moyoni mwako:

Zaburi 86:12,13  Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, kwa moyo wangu wote, nitalitukuza jina lako milele.  Maana fadhili zako ni nyingi sana; umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

Ndiyo, yawezekana mambo hayaendi kama ulivyotazamia.  Lakini kama vile mtu mmoja aliwahi kusema, moyo wa shukrani unafungua macho yetu tuweze kuona mibaraka inayotuzunguka kila wakati.

Kwa hiyo, ukiwa na mashaka, umshukuru Mungu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy