Unaweza Kutegemea Uaminifu Wa Mungu?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 89:1,2,14 Fadhili za BWANA nitaziimba milele; kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako ... Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
Hivi huwa unafanyaje pale unapojikuta sehemu ngumu sana, ukijisikia kama uko peke yako? Nijibu!, huwa unafanyeje!?, huwa unavumilia tu au huwa unamlilia Mungu?
Hisia ya upweke ni sawa na mtu aliyeko ndani ya shimo ndefu tena lenye giza, na hali hii huwa inatokea mara nyingi kwa watu wengi kuliko tunavyofikiria. R.C. Sproul alikuwa mchungaji na mwanatheolojia maarufu karne ya 20, akawa pia mhubiri kwenye redio. Kwa hali hiyo, ni rahisi mtu kufikiri kwamba yeye alikuwa na mahusiano mazuri na Mungu masaa 24 kila siku za wiki.
Ukisikiliza kipindi chake cha au ukisoma mojawapo ya vitabu vyake vingi alivyoandika, anaonekana kama mtu anayejua mengi, akifundisha kwa ujasiri. Je!, itawezekanaje mtu kama yeye awe na mashaka kama wewe na mimi? Hmm.
Lakini yeye aliwahi kusema hivi, “Kuna wakati sisikii uwepo wa Mungu. Lakini ahadi zake hazitegemei hisia zangu; zimesimikwa juu ya uaminifu wake.”
Kuna wakati hisia zetu zinatuangusha; zinatuambia kwamba ,Mungu amekuacha.
Zaburi 89:1,2,14 Fadhili za BWANA nitaziimba milele; kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako … Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
Mungu ni upendo. Milele ni mwaminifu. Uaminifu wake hauna mwisho. Ni Mungu wa kweli na wa haki. Ndio maana unaweza kumtegemea hata kama hisia zako zimevurugika. Ndio maana unaweza kujua kwamba yuko pamoja nawewe hapo ulipo. Ndio maana unaweza kuimba milele fadhili zake na uaminifu wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.