Unifundishe Njia Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86:11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.
Je! Umewahi kutafuta njia pa kupitia ukiwa mahali ambapo hujazoea? Kaskazini ni wapi? Nitumieje ramani,? Stendi ya basi iko wapi? Hii basi inayokuja, je! Itanipeleka pale ninapohitaji kwenda?
Kwa kweli, kupotea haipendezi hata kidogo. Ila siku hizi, kwa wengi wetu, tumerahisishiwa kwa kutumia apps za Google Ramani, Waze, Apple Ramani na kadhalika, na kweli zinatusaidia kufika pale vizuri tunapotaka.
Laiti maisha yenyewe yangekuwa rahisi hivi! Tukifikia njia panda na ikibidi tufanye maamuzi – Je! Nipitie njia hii au njia ile? Je! Nimeshapitiliza? Nirudi nyuma au? Niende wapi? – Kuna wakati tunafanya maamuzi ya haraka-haraka lakini mara nyingi ni kubahatisha tu. Mara ingine tunaahirisha. Ikishindikana, basi tunaacha na kurudi nyuma.
Labda utafikiri kwamba nimechanganikiwa, lakini mimi ninaona kwamba kubahatisha maamuzi ya maisha hivi, sio sahihi. Labda mtazamo kama wakwangu ulimsukuma Daudi kuandika maneno yafuatayo:
Zaburi 86:11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; nitakwenda katika kweli yako; moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako.
Daudi alipitia makona mengi maishani mwake – maamuzi mengine katika mazingira ya kuhatarisha hata uhai wake – kuliko yale tunayokabiliana nayo sisi.
Kumbukumbu kwangu mimi binafsi: Nikiwa na mashaka nipitie wapi, nisikose kumwomba Mungu anifundishe njia yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.