Uovu Uliomo Ndani Yetu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wagalatia 2:20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Uovu ni mwingi sana ulimwenguni mwetu. Kiburi, ubinafsi, jeuri, ukatili … utengano katika jamaa, mataifa wakipigana, maskini na waliotengwa kutupwa pembeni kama takataka. Kwa kweli, ni mwingi mno.
Lakini je! Ni kuhusu uovu uliomo ndani ya mioyo yetu sisi wenyewe? Labda utasema, “Subiri kwanza, mimi si mwovu.” Lakini hakuna aliye mkamilifu. Sote tunachezea uovu. Kama vile mwandishi Mrusi aitwaye Aleksandar Solzehnitsyn alivyoandika katika kitabu chake kiitwacho “Mkusanyiko wa Visiwa Vingi Pamoja wa Gulag” …
Labda wangekuwa waovu sehemu fulani wanadhuru kwa siri na ingetakiwa kuwatenganisha na jamii na kuwaangamiza. Lakini mstari uanotenganisha mema na mabaya kumbe! Unapita katikati ya moyo wa kila mwanadamu. Sasa, ni nani atakubali kuangamiza sehemu ya moyo wake mwenyewe?
Ni swali nyeti. Ndiyo maana Yesu anatuita tuchukue msalaba wetu na kumfuata. Ndiyo maana anatwambia kujitoa kabisa na kufisha nafsi zetu ili tuweze kupata uzima wa kweli. Mtume Paulo alieleza hivi:
Wagalatia 2:20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Ukitafakari habari ya ule mstari unaopita katikati ya moyo wako, mstari wa kutenganisha mema na mabaya, acha nikuulize, je! Umekata shauri la moja kwa moja kukubali kusulubiwa pamoja na Kristo, kutoa uhai wako ili na wewe uweze kutangaza kwamba, si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu?
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.