Moyo Wake wa Ukombozi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Sefania 3:16,17 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa, Usiogope, Ee sayuni; mikono yako isilegee. BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atakutuliza katika upendo wake, atakufarahia kwa kuimba.
Wakati tunapitia vipindi vigumu sana, tunaweza kujiuliza maswali magumu. Je! Nimeenda mbali sana? Je! Mungu bado ananipenda? Je! Amenichoka?
Watu teule wa Mungu, yaani watu wa Israel, mara nyingi walilimbuka wakiabudu miungu na kufanya mapatano na mataifa maovu, wasitende haki, wakiwapuuza maskini, wakizini, wakionyesha mara tena kwamba walikosa imani kwa Mungu aliyewatoa katika nchi ya Misri na kuwaingiza kwenye nchi ya Ahadi.
Karibia Agano la Kale lote ni orodha unaohuzunisha ya jinsi Israeli walivyoanguka wakidhihirisha jinsi walivyoshindwa kumheshimu Mungu. Sio wao tu, bali ni kama walikuwa mfano wa binadamu wote. Kuna kipindi fulani zamani zile, wakati Mungu alitangazi hukumu yake kali juu ya Yerusalemu.
Sefania 3:1,2 Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake.
Lakini hata hivi, baada ya muda mfupi tu, Mungu anatabiri mambo yafuatayo ambayo yanawahusu:
Sefania 3:16,17 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa, Usiogope, Ee sayuni; mikono yako isilegee. BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atakutuliza katika upendo wake, atakufarahia kwa kuimba.
Kutoka kwenye dhambi na hukumu na matokeo mabaya halafu … kuingia kwenye habari ya kuwatia moyo, kutangaza ushindi, furaha na hata kuimba. Ni mfumo unaorudiwarudiwa. Kwa nini? Kwa sababu Mungu anatupenda.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.