Upasuaji Mkubwa Unaohitajika
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamanye na kuziacha atapata rehema.
Wengi wetu tunaweza kutenganisha mema na mabaya. Sasa huwa tunajaribu kutenda mema kuliko mabaya. Tuzidi kidogo kutenda mema. Tupunguze maovu. Labda hii itatosha.
Ebu fikiria ingekuaje kama unaenda hospitali kutolewa donda ndugu. Je! Ungependa daktari atibu donda lote au nusu? Naona jibu ni wazi, si kweli? Atibu donda lote tafadhali! Kwa kawaida, bingwa wa upasuaji yeye huzidisha kidogo kwa kufika ndani ya nyama inayozunguka bacteria ili ahakikishe donda lote limetibiwa.
Turejee sasa kwa swala letu la mema na mabaya. dhambi, kama vile kansa, itakuwa na dalili zinazoonekana haraka na matokeo yake yataathiri ustawi … na hatimaye utakufa.
Ni dhahiri kwamba, zoezi la kuzidi kutenda mema kidogo ili ufunike mabaya machache yanayobaki huku ukitegemea kwamba hakuna atakayejua (hata Mungu asijue) … halitakuokoa, Itakuwa ni kama vile kutibu nusu ya kidonda, wala huwezi kupona.
Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamanye na kuziacha atapata rehema.
Mstari huu unasema, Njia pekee yaw ewe kuacha dhambi zako, nikutubu. Wala hakuna neno lolote tunaloweza kutumia zaidi ya KUTUBU. Kutubu ni zoezi la mtu binafsi kutambua na kukiri dhambi zake, kujutia kabisa tendo alilolifanya, kutafuta msamaha wa Mungu na kukata shauri kwamba atabadilisha mwenendo wake huko mbeleni.
Acha niseme tena, kupunguza-punguza dhambi si toba. Bali kuacha dhambi ni kutubu kweli kweli.
Yeye aziungamanye dhambi zake na kuziacha atapata rehema.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.