Upatane na Yaliyopita
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yalyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele …
Ebu fikiria kidogo kwamba wewe ni mwanajeshi anayeenda vitani. Ni swala la kuuawa au kusalimika. Lakini wakati ulitaka kuondoka kutoka nyumbani, ulizozana vibaya na mke wako. Swali, Je! Uko tayari kweli kukabiliana na adui?
Ni kweli, najua ni swala la nadharia tete, lakini najua kwamba unaweza kuifikiria, si kweli? Unaingia vitani na kuhatarisha maisha yako na umetoka nyumbani ukimfokea mtu yule ambaye unampenda zaidi ya wote.
Tukio kama hilo lingevuruga sana mawazo ya mwanajeshi akiingia mstari ule wa kurushiana risasi. Na ndivyo ilivyo katika maisha ya kila siku. Kama hutengenezi na kufanya amani na mambo yaliyopita wakati unakumbana na majuto yako, basi yataendelea kukusumbua kila siku huko mbeleni. Hairidhishi kuishi hivyo, hata kidogo. Sikiliza alivyoandika Mtume Paulo …
Wafilipi 3:13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele …
Yaani, Paulo alikuwa na mengi sana ya kujutia kuliko sisi sote. Kabla hajakutana na Yesu njiani kwenda Dameski, alikuwa anatesa Wakristo bila huruma. Wengi walikufa kwa mkono wake. Halafu siku moja alikutana na Yesu, , acha nikwambie, yesu anabadilisha kila kitu.
Kwa hiyo ukitathmini majuto yako, ukijaribu kutuliza na kupatana na yaliyopita, maneno hayo yajae moyo wako:
Natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.