Upendo Haupungui Neno Wakati wo Wote
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 13:8,13 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika ... Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo
Wewe na mimi tunao tabia kulenga mambo ambayo hatimaye hayana maana sana. Sasa kama hatimaye hayana faida, inabidi mtu ajiulize, je! Kwa nini niyape kipaumbele sasa?
Nina rafiki moja ambaye mke wake, baada ya watoto wao kuwa watu wazima, alimwarifu kwamba anaondoka sasa. Hakutoa sababu maalum. Mke wake alitaka kuanza upya tu.
Wakati alikuwa anafunga mizigo yake ndani ya katoni, vitu ambavyo viliwahi kuwa na thamani kwake, kweli alisumbuka sana. Lakini baba yake mzee alimpa ushauri mwenye busara. “Mwanangu,” alisema, “ni vitu tu.”
Je! Umewahi kusimama na kutafakari kuhusu jinsi unaweza kuwa umewekeza sana ndani ya vitu ambavyo havina maana, vitu ambavyo havitadumu? Ajira yako, vipaji ulivyo navyo, sifa zako katika jamii … vitu ambavyo havidumu … wakati kuna jambo moja ambalo tunaopenda kulisahau na kuacha pembeni. Jambo ambalo litadumu kuliko hivyo vingine vyote.
1 Wakorintho 13:8,13 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika … Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Ukiendelea na safari yako na kuelekea pale utakapoishi milele, acha nikusihi usilenge zaidi vitu vinavyoisha na kupata hasara ya vitu vidumuvyo. Usiruhusu kilicho bora kipishe kilicho kidogo; usiruhusu upendo upishe vitu tu.
Kwa sababu hayo mengine yote yataisha. Lakini upendo, lililo kuu kuliko vyote, hautaisha milele. Uishi maisha ya upendo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.