Usahihi Katika Teolojia Hautoshi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala mengine msiyaache.
Watu wanaielewa Habari Njema ya Yesu kwa njia mbali mbali. Mimi binafsi ni mtu wa kawaida tu. Ninafungua Biblia, ninaisoma na kuamini anachokisema Mungu hata kama kinaenda kinyume na mfumo wa kisasa wa ulimwengu huu.
Siwezi kudai kwamba mimi ni mwanathiolojia, hapana. Sina akili ya kutosha. Lakini nina shauku kubwa kwa ajili ya Neno la Mungu. Nataka kuzama zaidi, kuzidi kumkaribia Yesu, nizidi kumjua na kuwa kama aliyekusudia niwe wakati aliniumba. Hayo yote ni sawa kabisa … ila kuna hatari.
Hatari ni kwamba mtu anaweza kuwa na shauku kubwa kuhusu teolojia yake hadi anaitangaza sana akiacha kilicho muhimu zaidi. Upendo. Ni kwa sababu kadiri mtu anachunguza Neno la Mungu kwa undani, ndipo uovu wa watu wengine walioko huko unazidi kubainika.
Yesu alikutana na watu wa namna hiyo. Kulikuwa hata dhehebu ya dini ya watu waliojidai haki na hao ndiyo walipanga njama ya kumwangamiza Yesu. Yafuatayo ni sehemu ya maneno aliyeweza kusema juu yao:
Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala mengine msiyaache.
Jamaa hawa walitengeneza kanuni juu ya kanuni za ajabu-ajabu katika jitihada zao za kufuata Sheria ya Musa. Lakini waliacha kilicho muhimu zaidi. Upendo kupitia njia ya adili, rehema na uaminifu.
Usianguke ndani ya mtego. Kama vile mtu fulani alivyosema, telolojia sahihi haiwezi kufidia chuki za moyoni.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.