Ushahidi wa Imani Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 14:21,23 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake ... Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Sijui kama umewahi kujiuliza kama watu wengine wameshagundua kwamba uko tofauti na wengine? Labda wakishuhudia upole wako, wema wako, unyenyekevu na ukunjufu wako … hekima yako. Au pengine hawavioni ndani yako?
Hii ni changamoto, hususani ukijiita “Mkristo”. Kwa vyovyote, lazima uwe tofauti. Utofauti huo unadhihirika katika utii wako, hata kama hutaki kunisikiliza kwa hilo.
Yohana 14:21,23 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake … Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Ni kweli, hatuokoki kwa kumtii Yesu, ila utiifu wetu ni thibitisho, ni ushahidi wa imani yetu. Ina maana, tunadhihirisha imani yetu kwa kumtii Mungu. Lakini kama vile A.W. Tozer alivyosisitiza kwakusema, ‘kufikiri kwamba mtu anaokoka kwa matendo yake ni kosa la kutangaza wokovu bila utiifu.”
Tunaanza kutofautina na wengine pale tunapokuwa na furaha, upendo na wema, tunatii yale Yesu aliyotuamuru. Lakini mtu hawezi kufaulu kufanya hivyo peke yake, hata kidogo!
Ndio maana, mtu akidhamiria kumtii Yesu, uwepo wake unamjaza pamoja na utukufu ambao wengine hawawezi kukosa kuuona; anajazwa na upendo hata kwa watu ambao ni vigumu kuwapenda; anajazwa na wema ambao hautokani na yeye mwenyewe.
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.