... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ushirikiano Wenye Nguvu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; bali BWANA huziongoza hatua zake.

Listen to the radio broadcast of

Ushirikiano Wenye Nguvu


Download audio file

Ushirikiano katika kazi, yaani kuwa timu ya watu mbali mbali, kila mtu akileta mtazamo wake na kipaji chake na uzoefu wake; wote wakifanya kazi kwa pamoja na kulenga hatima moja, kwa kweli ni mfumo mzuri unaoleta maendeleo duniani, si kweli?

Hata kama kufanya kazi na watu wengine inasumbua mara kwa mara –hata hivi, uwezo wa kundi kufaulu kufanya mengi ni zaidi kuliko mtu pekee, huu ni ukweli usiopingika kabisa.

Mfano, leo hii unasikiliza kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA katika lugha hii kupitia chombo hiki cha usambazaji wa habari.  Ujumbe huu unaweza kukufikia kwa sababu ya timu yetu nzuri inayofanya kazi kwa pamoja.

Ni kweli, mgogoro hauna budi kutokea mara kadhaa – ila namshukuru Mungu kwamba kwenye kundi letu ni mara chache sana.  Lakini mitazamo na vipaji mbali mbali vinasababisha (a) makosa yapungue, halafu pia (b) matokeo yawe bora.  Ebu fikiria ingekuaje kuwa na Mungu Mwenyewe katika timu yenu!

Ila naona nimeeleza visivyo, si kwamba Mungu anajiunga na timu yetu, bali inabidi sisi tujiunge na timu yake Mungu.  Hii inasikika vizuri zaidi, si kweli?  Na hilo ndilo lengo Mungu alilo nalo:

Mithali 16:9  Moyo wa mtu huifikiri njia yake; bali BWANA huziongoza hatua zake.

Je!  Umewahi kuketi mezani katika kundi la watu mkipanga jambo fulani?  Inapendeza, sana,  Lakini ebu fikiria kama katika kupanga mambo na hatimaye kuyaweka katika utendaji, Mungu angekuwepo; Mungu angeongoza hatua zenu.  Je!  Si ingelikuwa bora kabisa?!

Usiache kupanga yale ambayo unataka kuyafanya, lakini umpishe Mungu aweze kuongoza hatua zako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy