Ushuhuda Wenye Nguvu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 1:17 Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Wanasiasa wanapokosa uhakika kuhusu jambo fulani walipeleke kwenye sera ipi, mara nyingi huwa wana tabia ya kurudia kanuni za zamani, kwamba, “ukiwa na mashaka, basi fuata yanayokupa faida.” Si kila wakati wanafanya hivyo, lakini ni mara nyingi tu.
Kwanini kujinufaisha? Ni kwasababu karibu watu wote wana ubinafsi kabisa, sera mpya ya serikali inapotangazwa; swali la kwanza linalokuja katika fikra zetu huwa ni hili, “Je! Hii itanisaidiaje? Itaingiliaje katika uhuru wangu, au itagusaje mapato yangu au maisha yangu?
Kutetea ubinafsi wa watu unaweza kusaidia mtu kupata kura nyingi na kushinda katika uchaguzi, lakini mara nyingi kunaleta sera mbaya. Na ndivyo ilivyo katika maisha yetu. Ni kweli, tunajitanguliza, kitu ambacho si kibaya kama hatuvuki mpaka. Lazima wewe na mimi tuhakikishe nyumbani tuna riziki, sehemu salama ya kuishi, tunasomesha watoto na kuwalea katika maadili na kadhalika. Inaeleweka kabisa, lakini …. tunapojitanguliza kwenye mahitaji huwa tunaingia kwenye tamaa zetu, na ni hatari.
Nataka hiki, nataka kile, nataka starehe, nataka mali, nataka kutalii, nataka, nataka, nataka. Sasa, tukiwa na mtazamo kama huo, ni dhairi kwamba matamanio yetu yatasababisha tusijali mahitaji ya msingi ya watu wenye hali duni wanaotuzunguka. Muda umefika wa kujikagua upya:
Isaya 1:17 Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Kuna watu tunawajua, watu ambao hawako mbali nasi, watu wenye uhitaji wa msaada kabisa. Kuna wakati wanahitaji jambo rahisi kama vile kuwasaidia na kuwatendea haki, hata kama liko kinyume cha ubinafsi wetu, tunahaja ya kusimama kidete na kuwatetea.
Ile tabia ya kujitanguliza isisababishe uache kujali wanyonge.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.